Athari Za Sayansi Na Teknolojia Katika Hadithi Za Watoto: Mifano Ya Ngano Kutoka Wilaya Ya Micheweni Pemba

IKISIRI

Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza hadithi za watoto, kwa kuangalia jinsi hadithi hizo zilivyoathiriwa na maendeleo ya sasa ya sayansi na teknolojia. Hususan, kwa kuchunguza mifano ya hadithi za ngano kutoka Wilaya ya Micheweni Zanzibar.

Utafiti ulibaini kwamba, sifa nyingi za Fasihi Simulizi zimebadilika au zimo katika mabadiliko makubwa. Hasa hasa katika kipindi hiki cha kukua na kuimarika kwa sayansi na teknolojia. Ikiwa hivyo ndivyo, basi ni dhahiri kwamba Fasihi Simulizi na vipera vyake inafaa vizidi kuchunguzwa zaidi, ili kujua ni kwa namna gani vipera hivyo vimeathiriwa na maendeleo hayo ya sayansi na teknolojia.

Utafiti huu umeongozwa na malengo matatu, ambayo ni kuchunguza madhara yanayotokana na sayansi na teknolojia jinsi yanavyoathiri usimuliaji na uhifadhi wa hadithi za watoto, hususan hadithi za ngano, kutathmini mchango wa sayansi na teknolojia katika maendeleo ya utanzu wa hadithi za watoto, kwa kuangalia mifano ya ngano kutoka Wilaya ya Micheweni Zanzibar na lengo la tatu ni kuchunguza mwamko wa wanajamii wa Wilaya ya Micheweni walioupata kuhusiana na athari ya sayansi na teknolojia katika utanzu wa hadithi za watoto, kwenye mifano ya hadithi za ngano. Katika malengo matatu hayo kila lengo lilipewa nafasi kutegemea na matokeo ya utafiti wenyewe.

Katika tasnifu hii, mkabala uliotumika ni wa nadharia ya Uhalisia. Nadharia hii imekuwa na umuhimu mkubwa sana katika kupata matokeo bora ya utafiti huu. Kwani nadharia hii ya uhalisia imetusaidia katika kujiridhisha kwamba, kila lengo tulilolijadili linasawiri uhalisi uliopo katika jamii ambayo ililengwa kufanyiwa utafiti.

Matokeo ya utafiti huu ni kwamba, utatoa mchango mkubwa katika uga huu wa Fasihi Simulizi kwani ni sehemu muhimu ya chanzo cha taarifa za kifasihi. Utafiti huu unategemewa pia kuwa na faida kubwa kwa taifa, kwani utasaidia kufafanua hadithi za watoto, kwa kuangalia mifano ya ngano ambazo, kwa kiasi fulani, zinaelekea kupotea kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Pia utasaidia kuzifanya hadithi hizo zisambae na kufahamika na watu wengi ndani na nje ya nchi yetu.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Mbarouk, M (2021). Athari Za Sayansi Na Teknolojia Katika Hadithi Za Watoto: Mifano Ya Ngano Kutoka Wilaya Ya Micheweni Pemba. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/athari-za-sayansi-na-teknolojia-katika-hadithi-za-watoto-mifano-ya-ngano-kutoka-wilaya-ya-micheweni-pemba

MLA 8th

Mbarouk, Mbarouk "Athari Za Sayansi Na Teknolojia Katika Hadithi Za Watoto: Mifano Ya Ngano Kutoka Wilaya Ya Micheweni Pemba" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://track.afribary.com/works/athari-za-sayansi-na-teknolojia-katika-hadithi-za-watoto-mifano-ya-ngano-kutoka-wilaya-ya-micheweni-pemba. Accessed 05 Nov. 2024.

MLA7

Mbarouk, Mbarouk . "Athari Za Sayansi Na Teknolojia Katika Hadithi Za Watoto: Mifano Ya Ngano Kutoka Wilaya Ya Micheweni Pemba". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 05 Nov. 2024. < https://track.afribary.com/works/athari-za-sayansi-na-teknolojia-katika-hadithi-za-watoto-mifano-ya-ngano-kutoka-wilaya-ya-micheweni-pemba >.

Chicago

Mbarouk, Mbarouk . "Athari Za Sayansi Na Teknolojia Katika Hadithi Za Watoto: Mifano Ya Ngano Kutoka Wilaya Ya Micheweni Pemba" Afribary (2021). Accessed November 05, 2024. https://track.afribary.com/works/athari-za-sayansi-na-teknolojia-katika-hadithi-za-watoto-mifano-ya-ngano-kutoka-wilaya-ya-micheweni-pemba

Document Details
Mbarouk Juma Mbarouk Field: Linguistics Type: Dissertation 124 PAGES (26714 WORDS) (pdf)