SHUKURANI
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa taasisi na watu mbalimbali waliotoa ushauri na michango yao ya hali na mali iliyowezesha kukamilisha kazi hii. Awali ya yote, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kumshukuru Mwenyezi-Mungu (sw) kwa kunijaalia afya njema katika kipindi chote cha masomo yangu. Afya ambayo iliniwezesha kuikamilisha tasnifu hii kwa muda mwafaka. Kwanza, namshukuru msimamizi wangu, Dkt. Athumani S. Ponera, ambaye licha ya majukumu mengi mengine yaliyomkabili lakini alijitolea kuniongoza na kunishauri hatua kwa hatua hadi kuikamilisha kazi hii. Ahsante kwa msaada wako usioweza kulipika kwa kitu chochote cha thamani ila Mungu akulipe kheri kwa kukuingiza peponi. Amin. Pili, nawashukuru wahadhiri wangu wote, hasa Dkt. A. S. Ponera na Dkt. R. Y. Sebonde, kwa mwongozo walionipa katika kipindi chote nilichokuwa darasani kwa masomo. Tatu, nawashukuru wanafunzi wa shahada ya kwanza wanaosoma fasihi ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Dodoma, Chuo cha Kumbukumbu ya Abdul-Rahmani Sumeiti na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, kwa ushirikiano na mchango mkubwa walionipa hadi kukamilika kwa tasnifu hii. Kwani bila ya ushiriki wao ukusanyaji wa data usingekuwa na ufanisi. Nne, shukurani za pekee zimwendee mke wangu, Mossi M. Ame, pamoja na watoto wangu, Khairat, Fatma, Husna, Abdul-latwifu na Mudrik, kwa uvumilivu mkubwa waliouonesha katika kipindi chote cha masomo yangu. Nawapa hongera kwa utulivu, msaada na mchango mkubwa walionipa. Kwa hivyo, nakiri na kuuthamini mchango wa hali na mali wa kila aliyenisaidia hata kwa kiwango kidogo. Mungu atulipe na aturahisishiye kila lenye manufaa ya dunia na akhera. Amin.
Makame, S (2021). Matumizi Ya Falsafa Ya Usihiri Katika Riwaya Teule Za Euphrase Kezilahabi. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-falsafa-ya-usihiri-katika-riwaya-teule-za-euphrase-kezilahabi
Makame, Silima "Matumizi Ya Falsafa Ya Usihiri Katika Riwaya Teule Za Euphrase Kezilahabi" Afribary. Afribary, 21 May. 2021, https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-falsafa-ya-usihiri-katika-riwaya-teule-za-euphrase-kezilahabi. Accessed 28 Dec. 2024.
Makame, Silima . "Matumizi Ya Falsafa Ya Usihiri Katika Riwaya Teule Za Euphrase Kezilahabi". Afribary, Afribary, 21 May. 2021. Web. 28 Dec. 2024. < https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-falsafa-ya-usihiri-katika-riwaya-teule-za-euphrase-kezilahabi >.
Makame, Silima . "Matumizi Ya Falsafa Ya Usihiri Katika Riwaya Teule Za Euphrase Kezilahabi" Afribary (2021). Accessed December 28, 2024. https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-falsafa-ya-usihiri-katika-riwaya-teule-za-euphrase-kezilahabi