Taswira Katika Ngano Za Kiswahili Kutoka Wilaya Ya Kusini Unguja-Zanzibar

SHUKRANI

Shukrani za awali ziende kwa Mwenyezi Mungu, muumba wa viumbe vyote, kwa kunisaidia kwa uwezo wake mkubwa kunilinda na kunipa afya katika kipindi chote cha kufanya utafiti huu mpaka ukakamilika. Shukrani nyingine ni kwa msimamizi wangu wa utafiti huu Dkt. Muhammed Seif Khatib kwa kuniongoza, kunishauri na kunipa changamoto mbalimbali za kutafuta taarifa zaidi na zaidi. Mungu mzidishie baraka na kumlinda na mabaya yote ya dunia. Wahadhiri wangu wote kwa kuwa nao pamoja tangu mwanzo wa masomo hadi kumaliza kwake. Kwa kuwa wao wamenisaidia kupata taaluma na maarifa yaliyoniwezesha kuufanya utafiti huu. Miongoni mwao ni Prof. Madumulla, Dkt. Ponera na Dkt. Sebonde Rafiki. Kadhalika shukrani zangu za dhati ni kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kunidhamini na kuniruhusu kuchukua mafunzo haya. Pia watendaji na wasimamizi wote wa asasi zote ambazo nazo kwa kiasi kikubwa zilishirikiananami bega kwa bega kwa kuniongoza na kunishauri kila ilipobidi. Asasi hizo ni Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raisi, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar, Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA), Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na skuli zote za sekondari zilizoshiriki katika utafiti huu. Pia namshukuru mume wangu Hamid Haji Makamekwa kuniruhusu kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Dodoma shahada ya Uzamili na kuniruhusu kwa muda mrefu kukusanya data za utafiti huu uwandani. Shukrani nyingine ziende kwa wanafunzi wenzangu wa shahada ya Uzamili ya Fasihi ya Kiswahili 2013/2014 na wengine wengi ambao nilishirikiana nao katikakufanikisha utafiti huu. Mwisho, nawashukuru wakaziwa vijiji vya Wilaya ya Kusini vilivyofanyiwa utafiti. Aidha ni vigumu kumshukuru mmoja mmoja kwa washiriki wote, hata hivyo, shukrani kwa wote walioshiriki katika kuifanikisha na kuikamilisha kazi hii.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Mwinyi, H (2021). Taswira Katika Ngano Za Kiswahili Kutoka Wilaya Ya Kusini Unguja-Zanzibar. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/taswira-katika-ngano-za-kiswahili-kutoka-wilaya-ya-kusini-unguja-zanzibar

MLA 8th

Mwinyi, Hassina "Taswira Katika Ngano Za Kiswahili Kutoka Wilaya Ya Kusini Unguja-Zanzibar" Afribary. Afribary, 01 May. 2021, https://track.afribary.com/works/taswira-katika-ngano-za-kiswahili-kutoka-wilaya-ya-kusini-unguja-zanzibar. Accessed 24 Nov. 2024.

MLA7

Mwinyi, Hassina . "Taswira Katika Ngano Za Kiswahili Kutoka Wilaya Ya Kusini Unguja-Zanzibar". Afribary, Afribary, 01 May. 2021. Web. 24 Nov. 2024. < https://track.afribary.com/works/taswira-katika-ngano-za-kiswahili-kutoka-wilaya-ya-kusini-unguja-zanzibar >.

Chicago

Mwinyi, Hassina . "Taswira Katika Ngano Za Kiswahili Kutoka Wilaya Ya Kusini Unguja-Zanzibar" Afribary (2021). Accessed November 24, 2024. https://track.afribary.com/works/taswira-katika-ngano-za-kiswahili-kutoka-wilaya-ya-kusini-unguja-zanzibar