SHUKRANI
Nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na utukufu aliyenipa nguvu, uhai, afya na uvumilivu hata nikaweza kuifanya kazi hii kwa kiwango kinachostahili. Pili, nimshukuru kwa nafasi ya pekee Profesa. Frowin Paul Nyoni, huyu ndiye msimamizi wangu wa utafiti huu. Natambua majukumu mengi na mazito ya kikazi na ya kifamilia aliyonayo lakini alichukua na alitumia muda wake mwingi pia katika kuisoma na kutoa mchango wake ili kuleta ufanisi wa kazi hii, tangia tulipoianza katika hatua ya pendekezo la utafiti mpaka wakati wa uandishi wa tasnifu hii. Hakika mchango wake nina uthamini sana. Tatu, nawashukuru pia walimu wangu, Profesa Joshua S. Madumulla, Profesa Lakshmanan, Dkt Elias M. Songoyi, Dkt Rafiki Y. Sebonde na Bw. Athuman Ponera ambao wamenifundisha katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kunipa misingi thabiti ya Fasihi ya Kiswahili. Nne, nichukue pia nafasi hii kumshukuru Mkuu wa Idara ya Fasihi, Mawasiliano na Uchapaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na timu yake kwa ujumla kwa kutoa kibali cha kuruhusu kutumika kwa makavazi yanayopatikana katika Maktaba yao. Pia kutoa maelekezo yaliyo kuwa muhimu kwangu katika zoezi zima la ukamilishaji wa andiko hili. Tano, shukrani zangu za dhati ziwaendee wale wote walionipa ushirikiano katika kipindi chote cha ukusanyaji wa data za utafiti huu, ni vigumu kuwataja mmoja mmoja kutokana na idadi yao kuwa kubwa lakini kwa uchache wao, namshukuru ndg, Kwame Elly Anangisye (katibu wa mbunge jimbo la Mbeya Mjini), Mkuu wa v shule ya sekondari Sinde- Mbeya, Mwl Eston A. Mbilinyi wa Sinde sekondariMbeya pamoja na wanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Sinde- Mbeya. Namshukuru pia mkurugenzi wa Kiss Library iliyopo Mwanjelwa Mbeya. Lakini nitakuwa mnyimi wa fadhila kama sikutumia nafasi hii kumshukuru Bw. Deogratias J. Kiswaga kwa msaada wake katika mambo ya kiufundi wa kielektroniki katika mchakato wa uandishi wa kazi hii. Sita, nawashukuru pia ndugu na jamaa ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa msaada kwangu katika hatua mbalimbali za uandishi wa kazi hii tangu hatua ya mwanzo ya kuandika mada ya utafiti mpaka hatua ya mwisho ya uandishi wa tasnifu hii. Saba, namshukuru kwa nafasi ya pekee mama yangu mzazi, Bi S.B.Sanga kwa kunizaa na kunilea katika hatua mbalimbali za makuzi ya binadamu. Hakika anastahili sifa, kwani yeye ndiye dira ya maisha yangu.
Sanga, E (2021). Dhima Ya Nyimbo Za Bongo Fleva Zihusuzo Rushwa Katika Kuleta Mabadiliko Kwa Jamii. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/dhima-ya-nyimbo-za-bongo-fleva-zihusuzo-rushwa-katika-kuleta-mabadiliko-kwa-jamii
Sanga, Edomu "Dhima Ya Nyimbo Za Bongo Fleva Zihusuzo Rushwa Katika Kuleta Mabadiliko Kwa Jamii" Afribary. Afribary, 29 Apr. 2021, https://track.afribary.com/works/dhima-ya-nyimbo-za-bongo-fleva-zihusuzo-rushwa-katika-kuleta-mabadiliko-kwa-jamii. Accessed 28 Dec. 2024.
Sanga, Edomu . "Dhima Ya Nyimbo Za Bongo Fleva Zihusuzo Rushwa Katika Kuleta Mabadiliko Kwa Jamii". Afribary, Afribary, 29 Apr. 2021. Web. 28 Dec. 2024. < https://track.afribary.com/works/dhima-ya-nyimbo-za-bongo-fleva-zihusuzo-rushwa-katika-kuleta-mabadiliko-kwa-jamii >.
Sanga, Edomu . "Dhima Ya Nyimbo Za Bongo Fleva Zihusuzo Rushwa Katika Kuleta Mabadiliko Kwa Jamii" Afribary (2021). Accessed December 28, 2024. https://track.afribary.com/works/dhima-ya-nyimbo-za-bongo-fleva-zihusuzo-rushwa-katika-kuleta-mabadiliko-kwa-jamii