IKISIRI
Utafiti ulichunguza matumizi ya lugha katika methali kwa kujiegemeza katika
methali za Kinyakyusa kama mfano. Methali kama utanzu wa Fasihi Simulizi wenye
hekima unaoeleza kwa ufasaha wa lugha kwa ufupi wenye kufurahisha, una
umuhimu sana katika jamii katika kuelimisha. Kipengele hiki hakijatafitiwa kwa kina
katika methali za Kinyakyusa.
Taarifa za utafiti huu zilikusanywa kwa njia ya usaili, dodoso na mjadala wa kikundi
katika mkoa wa Mbeya wilaya ya Kyela. Uchunguzi wa taarifa za utafiti
zilizokusanywa uliongozwa na nadharia ya Umuundo ambayo ni miongoni mwa
nadharia za uhakiki wa kazi za Fasihi inayochambua kazi ya Fasihi kwa kuichunguza
kazi yenyewe. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa njia ya ufafanuzi.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba matumizi ya methali katika jamii ya
Bhanyakyusa yameanza kupotea kutokana na muingiliano mkubwa na jamii
zinazotumia lugha tofauti na Kinyakyusa. Pia, imedhihirika kuwa uteuzi wa maneno
yanayotumika katika methali huzingatia dhima ya methali inayotambwa katika
kujenga picha na ishara kwa jamii. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa methali za
lugha ya Kinyakyusa zinapotumiwa miongoni mwa wanajamii kunakuwepo na athari
chanya kwa wamilisi wa lugha hiyo; pamoja na athari hasi kwa wale wasio na umilisi
wa kutosha juu ya lugha hiyo. Jambo hili linahatarisha kupotea kwa matumizi ya
utanzu huu miongoni mwa Bhanyakyusa.
Utafiti huu una mchango mkubwa katika taaluma ya Fasihi Simulizi kwani ni
sehemu ya kutunza amali za jamii. aidha, unatoa changamoto kwa watafiti
kujishughulisha na methali na Fasihi Simulizi kwa ujumla ili kuiepusha na upotevu
unaotokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Philip, D (2021). Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa
Philip, Daud "Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa. Accessed 25 Dec. 2024.
Philip, Daud . "Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 25 Dec. 2024. < https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa >.
Philip, Daud . "Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa" Afribary (2021). Accessed December 25, 2024. https://track.afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa