Matumizi Ya Utanzia Katika Riwaya Pendwa Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Ben Mtobwa Na Hussein Tuwa

IKISIRI

Tasnifu hii ilijigeza katika kuchunguza matumizi ya utanzia katika riwaya pendwa za

Kiswahili ulinganisho wa riwaya za Ben Mtobwa na Hussein Tuwa. Ponera (2014)

anasema kuwa utanzia ni mbinu ambayo mtunzi hutumia vipengele mbalimbali

vizuavyo huzuni, masikitiko, jitimai na mateso kwa hadhira yake. Vipengele hivyo

huweza kujengwa na mateso, ugumu wa maisha, vifungo, mabaa kama vile njaa,

gharika, kimbunga, magonjwa, ulemavu (wa viungo au michakato ya mwili, pamoja

na ule wa mifumo ya mwili kama vile ugumba, utasa).

Mapitio yaliyotumika katika tasnifu hii yaligawanyika katika makundi mawili. Kundi

la kwanza, mapitio yanayohusiana na utanzia, na kundi la pili, mapitio

yanayohusiana na riwaya pendwa. Mbinu iliyotumika ni udurusu maktabani pamoja

na usaili. Maeneo yaliyotumika kukusanyia data ni Dodoma na Dar es Salaam.

Nadharia iliyotumika ni uhalisia ambayo huchunguza utokeaji wa matukio ambayo

huendana na hali halisi ya ulimwengu.

Matokeo ya tasnifu hii yanaonesha kuwa utanzia upo katika kazi mbalimbali za

fasihi yaani, fasihi simulizi na fasihi andishi. Aidha, yanaonesha kuna aina tatu za

utanzia ambazo, ni utanzia wa kimwili, utanzia wa kisaikolojia na utanzia wa

kimaumbile. Pia, kuna vijenzi mbalimbali ambavyo vinaibua utanzia katika riwaya

teule na jamii kwa ujumla. Vilevile, matokeo ya tasnifu hii yanaonesha kuwa kuna

uhusiano wa moja kwa moja kati ya matukio ya kitanzia na matukio ya kifutuhi.

mpya wa kitaaluma katika fasihi ya Kiswahili kama ifuatavyo: Mosi, kubainika kwa

tofauti ya tanzia na utanzia. Pili, kuibuliwa kwa matukio ya utanzia ambayo

hujitokeza katika riwaya pendwa na si tamthiliya pekee. Tatu, kuibuliwa kwa aina

mbalimbali za utanzia zilizotumika na waandishi teule.