Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya

IKISIRI

Utafiti huu unahusu kuchunguza mielekeo ya watumiaji lugha ya Kiswahili kuhusiana na

ukinzani katika methali. Kwa mfano methali, Fuata nyuki ule asali na Fuata nyuki ufe

mzingani. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili; nadharia ya mguso na nadharia ya

umaanishaji. Katika upande wa ukusanyaji data, utafiti huu ulitumia hojaji kwenda nyanjani

na udurusu wa kina kuhusu methali za Kiswahili. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kubaini na

kuchanganua mielekeo ya wanafunzi na walimu wa fasihi ya kiswahili kuhusu kuwepo na

methali ambazo maana zake zinakinzana. Matokeo yalibaini kwamba idadi kubwa ya

watafitiwa ina mwelekeo chanya kuhusiana na suala lililotafitiwa. Baadhi ya sababu

zilizochangia watafitiwa kuwa na mwelekeo chanya ni pamoja na maoni kwamba methali hizi

zilizo na maana kinyume humsaidia mwanajamii kutafakari kabla ya kuchukua mwelekeo

fulani na labda kuepuka matatizo ya baadaye. Mojawapo ya majukumu ya methali ni

kushauri. Hivyo basi, ukinzani utakupa nafasi ya kuchagua ushauri unaokufaa binafsi na upi

wa kutupilia mbali. Aidha, kila methali huwakilisha hali halisi ya maisha. Maisha yenyewe

yamejaa hali kinzani kama vile urafiki/uadui, wema/ubaya, furaha/huzuni na kadhalika. Kwa

kuzingatia kauli hii, kila methali huwakilisha hali fulani. Kwa mujibu wa baadhi ya

waliotafitiwa, ukinzani huleta mwelekeo hasi. Walitetea kauli hii kwa kusema kuwa methali

zinapokinzana huzua utata na hali ya kumchanganya mtumiaji lugha asijue methali gani

itamfaa kwani moja inakuongoza huku, nayo nyingine inakutuma kule! Utafiti huu ulibaini

kuwa walimu wana changamoto kubwa sana wanapoelezea maana na matumizi ya methali

zinazobishana kwa wanafunzi wao. Asilimia mia moja ya walimu wa fasihi waliotafitiwa

walitoa changamoto wanazokumbana nazo wanaposomesha suala la ukinzani katika methali

za Kiswahili. Ubishi upo katika methali za Kiswahili lakini iwapo kila methali itatumika

katika muktadha, hali na kwa hadhira mwafaka suala la ubishi huu halitakuwa changamoto

kubwa. Jambo la msingi litakalozingatiwa ni maana (ufaafu) na matumizi ya methali

mahususi. Nadharia ya umaanishaji inashikilia kuwa fasihi inapaswa kuwa na maana. Maana

itapatikana baada ya kutumia kila methali katika muktadha na mazingira mwafaka, ndiposa

mguso au athari ya fasihi ipatikane (ili fasihi iweze kutekeleza jukumu lake katika jamii).

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

MBUSYA, C (2021). Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya

MLA 8th

MBUSYA, CATHERINE "Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya" Afribary. Afribary, 08 May. 2021, https://track.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya. Accessed 25 Dec. 2024.

MLA7

MBUSYA, CATHERINE . "Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya". Afribary, Afribary, 08 May. 2021. Web. 25 Dec. 2024. < https://track.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya >.

Chicago

MBUSYA, CATHERINE . "Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya" Afribary (2021). Accessed December 25, 2024. https://track.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya