IKISIRI
Tasnifu hii inahusu suala la malezi ya mtoto wa kike katika riwaya ya Kiswahili
ambayo ni miongoni mwa kazi za Fasihi Andishi zilizomakinikia jambo hili.
Tumepata kariha ya kufanya utafiti huu baada ya kuona kwamba kipengele cha
malezi ya mtoto wa kike, licha ya kusawiriwa katika riwaya ya Kiswahili,
hakijachunguzwa vya kutosha, huku mtoto wa kike akikabiliwa na changamoto
mbalimbali za kimalezi na kimazingira hasa katika zama hizi za utandawazi. Pia,
wazazi na walezi wanaonekana kukabiliwa na changamoto anuwai katika kuwalea
watoto wao wa kike.
Utafiti uliongozwa na malengo manne; kuchunguza mikitadha ya maisha ya
waandishi teule na athari zake katika kusawiri malezi ya mtoto wa kike, mifumo ya
malezi ya mtoto wa kike katika jamii za waandishi teule, kuwapo au kutokuwapo
kwa upatanifu wa vipengele vya malezi ya mtoto wa kike katika riwaya na maisha ya
jamii za waandishi teule, na kulandana na kutofautiana kwa vionjo vya malezi ya
mtoto wa kike katika riwaya teule za waandishi teule.
Data za msingi tulizipata kwa kudurusu riwaya teule, na fuatizi tulizipata uwandani
kupitia njia za udodosi, na mahojiano. Tumefanya utafiti katika mikoa ya Kaskazini
Pemba, Mjini Magharibi (Unguja), Mwanza, Dodoma, Dar es Salaam na Tanga.
Nadharia tuliyoitumia katika utafiti huu wa kifafanuzi ni ya Ufeministi sambamba na
mkabala wake wa Ufeministi wa ki-Afrika, ilituongoza katika kukusanya na
kuchanganua data.
Elimu ya malezi inahitajika kwa wazazi na walezi ili malezi kwa watoto wakiwamo
wa kike, yaendane na mabadiliko katika jamii ya sasa.
Mohamedi, R (2021). Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed
Mohamedi, Rasuli "Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed" Afribary. Afribary, 27 Apr. 2021, https://track.afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed. Accessed 19 Nov. 2024.
Mohamedi, Rasuli . "Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed". Afribary, Afribary, 27 Apr. 2021. Web. 19 Nov. 2024. < https://track.afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed >.
Mohamedi, Rasuli . "Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed" Afribary (2021). Accessed November 19, 2024. https://track.afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed