Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki

IKISIRI

Shughuli nyingi za kijamii hutumia lugha inayopata maana katika muktadha

inamotumika. Hali hii imechochea kutaka kujua namna Waisukha wanavyotumia lugha

kuendeleza ubabedume katika majigambo yanayoghaniwa kwenye sherehe za

upiganishaji fahali kisemantiki. Utafiti huu ulichunguza ubabedume miongoni mwa

Waisukha jinsi unavyodhihirika katika Majigambo ya Miviga ya Shilembe na Mchezasili

wa Mayo. Vipashio vya lugha vinavyosheheni ubabedume katika majigambo hayo

vilihakikiwa kwa mtazamo wa kisemantiki. Utafiti uliongozwa na madhumuni haya:

kupambanua vipashio vya lugha hususan nomino, vishazi na vitenzi katika majigambo ya

miviga ya Shilembe na Mchezasili wa Mayo vinavyodhihirisha ubabedume miongoni

mwa Waisukha kisemantiki, kuhakiki tamathali za usemi zinazosheheni ubabedume kwa

mtazamo wa kisemantiki na kutalii nafasi ya lugha, historia na itikadi za Waisukha katika

kujenga na kudumisha ubadedume. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili: Nadharia

ya UCHAMAWADI na Uwezo-Uume. Wachangiaji mashuhuri katika nadharia ya

UCHAMAWADI ni wataalam kama vile; Gee (1990), Fairclough (1992), Teun Van Dijk

(1993) na Wodak (2001). Iliwekewa msingi na kazi mbalimbali za wataalam hawa.

Hutambua uamilifu wa lugha katika jamii. Mihimili yake mikuu ni; uhakiki, uwezo au

mamlaka, historia na itikadi. Nadharia ya Uwezo-Uume iliasisiwa na Robert Bly (Well &

Holland, 2001) na kuendelezwa na Connell (1995). Inahusisha mahusiano ya wanawake

na wanaume katika jamii. Baadhi ya mihimili yake ni; itikadi za kijamii ambazo

huongoza fikra, mitazamo na mielekeo ya wanajamii kuhusu hali mbalimbali za kijamii.

Nadharia hizi zilitumiwa ili kuchangiana. Utafiti huu ulifanywa katika Kaunti Ndogo ya

Shinyalu, Kaunti ya Kakamega. Watafitiwa walikuwa fanani na washiriki katika sherehe

za Shilembe na Mchezasili wa Mayo. Usampulishaji ulifanywa kwa kutumia aina tatu.

Utafiti ulilenga kukusanya majigambo ishirini na saba kimaksudi kutegemea nasaba

ishirini na saba za Waisukha. Majigambo kumi na sita yalikusanywa kwa kutumia uteuzi

wa kimapokezano. Uteuzi wa kimaksudi ulitumiwa kuteua nasaba saba zilizo na

majigambo maarufu na uteuzi wa kinasibu ukatumiwa kuchagua majigambo tisa. Jumla

ya majigambo yaliyotumiwa yalikuwa kumi na sita. Mbinu za Uchunzaji-Shiriki na

Kiethnografia zilitumiwa na zilijumuisha kuishi na watafitiwa, kushiriki, kushuhudia

sherehe hizo pamoja na kuwahoji ili kukusanya majigambo hayo.Data iliwasilishwa na

kuchanganuliwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano, picha na vielelezo. Matokeo

yamebainisha kuwa, lugha ni kipengele muhimu cha jamii ya Waisukha kwa vile

humsawiri mwanamume Mwisukha kama aliye na mamlaka zaidi ya mwanamke. Hali hii

itafaidi jinsia ya kike kwa vile wanaume watayashughulikia majukumu yao kikamilifu

katika jamii. Utafiti umebainisha kuwa, uwezo wa mwanaume umetamalaki katika

majigambo ya Waisukha yaliyosheheni vipashio vya lugha kisemantiki. Unatarajiwa

kuupanua uwanja wa Fasihi Simulizi na Isimu kwa kulikuza suala la kuchanganua

majigambo, kipera ambacho ni muhimu katika Fasihi Simulizi kwa mtazamo wa

kisemantiki. Utafiti unatoa mchango katika kuelewa umuhimu wa Shilembe na

Mchezasili wa Mayo na mila, desturi na itikadi za Waisukha zinazowasilishwa kutoka

kizazi kimoja hadi kingine kupitia masimulizi ya Mwafrika.Utafiti huu unanuia

kuwachochea wasomi wa Fasihi Simulizi na Isimu wa baadaye kuchanganua Fasihi

Simulizi kwa kina zaidi kwa kuangazia vipashio vya lugha na kuzua

mwingilianotaaluma katika Kiswahili.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

, K & Lukamika, M (2021). Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki

MLA 8th

, Kibigo and Mary Lukamika "Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki" Afribary. Afribary, 07 May. 2021, https://track.afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki. Accessed 25 Dec. 2024.

MLA7

, Kibigo, Mary Lukamika . "Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki". Afribary, Afribary, 07 May. 2021. Web. 25 Dec. 2024. < https://track.afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki >.

Chicago

, Kibigo and Lukamika, Mary . "Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki" Afribary (2021). Accessed December 25, 2024. https://track.afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki