Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Tungizi Za Mnyagatwa Na Diwani Ya Midulu

IKISIRI

Utafiti huu ulichunguza ujaala katika ushairi wa Kiswahili huku uchunguzi na mifano vikitolewa katika diwani ya Tungizi za Mnyagatwa na Diwani ya Midulu zilizotungwa na Tigiti Sengo. Ujaala ni mtazamo ambao watunzi wa kazi za kifasihi huutumia katika kusana kazi zao. Dhana ya ujaala tumeitumia tukimaanisha hali ya viumbe kuishi kwa imani ya kuwa ipo kani inayoyaongoza na kuyatawala maisha yao hapa ulimwenguni. Dhana hii ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili haijachunguzwa vya kutosha; yumkini, hali hii inasababisha kutojulikana miongoni mwa hadhira ya kazi za fasihi.

Kwa kiasi kikubwa, utafiti ulifanyika maktabani. Vilevile, tulienda uwandani kwa ajili ya mahojiano na sampuli iliyoteuliwa. Data zilikusanywa katika miji ya Dodoma, Dar es Salaam na Tanga. Mbinu ya ufafanuzi ndiyo iliyotumika kutolea matokeo ya utafiti huu. Uchambuzi wa data umefanywa kwa kutumia nadharia ya ujaala kutokana na mihimili yake kufaa katika kubainisha aina za ujaala, fikra za kijaala katika diwani teule na kufafanua miktadha ya maisha ya mwandishi inavyohusiana na ujaala uliomo kwenye diwani zake teule.

Utafiti umebaini kuwa, ujaala ni mtazamo uliouathiri sana utanzu wa ushairi. Pia, kila jamii inaamini kuwapo kwa kani inayoyaongoza maisha yao ijapokuwa kuna tofauti ya namna ya kuichukulia au kuiita kani hiyo. Utafiti huu uliibua michango mipya kama vile kubainisha aina za ujaala kwa Watanzania pamoja na fikra zake. Pia, utafiti umedhihirisha kuwa miktadha ya maisha ya mwandishi ina uhusiano mkubwa na mawazo ya kijaala katika kazi yake. Utafiti umependekeza tafiti zaidi zifanyike juu ya falsafa ya ujaala katika riwaya na tamthiliya pamoja na kwenye tanzu za fasihi nenwa.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

HASSAN, H (2021). Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Tungizi Za Mnyagatwa Na Diwani Ya Midulu. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-tungizi-za-mnyagatwa-na-diwani-ya-midulu

MLA 8th

HASSAN, HASSAN "Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Tungizi Za Mnyagatwa Na Diwani Ya Midulu" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://track.afribary.com/works/ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-tungizi-za-mnyagatwa-na-diwani-ya-midulu. Accessed 25 Dec. 2024.

MLA7

HASSAN, HASSAN . "Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Tungizi Za Mnyagatwa Na Diwani Ya Midulu". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 25 Dec. 2024. < https://track.afribary.com/works/ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-tungizi-za-mnyagatwa-na-diwani-ya-midulu >.

Chicago

HASSAN, HASSAN . "Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Tungizi Za Mnyagatwa Na Diwani Ya Midulu" Afribary (2021). Accessed December 25, 2024. https://track.afribary.com/works/ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-tungizi-za-mnyagatwa-na-diwani-ya-midulu