Usawiriwa Vijanakatika Tamthilia Teuleza Kisw Ahili

IKISIRI

Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza ~awiri wa vijana katika tamthilia teule za Kiswahili.

Mtafiti amechanganua taswira mbali mbali zilizoibuka katika tamthilia hizi teule.

Imebainika kuwa, taswira hizi ni kiwakilishi cha njia wanazotumia vijana kujipa

mamlaka na kuyatumia, pamoja na mamlaka hayo kutumika kwao. Tasnifu hii

imeonyesha kuwa, vijana wana uwezo wa kujipa mamlaka na kuyatumia sawa na wazee

katikajamii. Hata hivyo, njia za kufanya hivyo ni tofauti na zile za wazee!

Nadharia ya Ki-Foucault imetumika katika kuchanganua taswira zilizoibuka katika

tamthilia teule. Nadharia hii huonyesha narnna ambavyo mahusiano ya kijamii husawiri

kinyang'anyiro cha matumizi ya mamlaka.

Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia vipengele vya kimsingi katika

tasnifu hii. Vipengele hivi vimeonyesha dhana muhimu kama zilivyotumiwa katika

utafiti huu, narnna suala la utafiti lilivyochipuka, malengo na misingi ya nadharia

iliyoongoza utafiti huu, mapitio ya maandishi na mbinu za utafiti zilizotumika.

Sura ya pili imejadili usawiri wa vijana katika asasi mbali mbali za kijamii. Katika sura

hii dhana ya kijana, utamaduni wa vijana, mielekeo kuwahusu vijana, na hali zao duniani,

zimefafanuliwa. Katika sura ya tatu, taswira za vijana katika tarnthilia za Wakati Ukuta (1971) na Uasi

(1980) zimechunguzwa. Tamthilia hizi zinawakilisha zile za awali katika utunzi wa

tamthilia ya Kiswahili.

Sura ya nne imechanganua taswira za vijana katika tamthilia za Kitumbua Kimeingia

Mchanga (2000) na Pango (2003). Tamthilia hizi ni kiwakilishi cha utunzi wa sasa

katika historia ya tamthilia ya Kiswahili.

Katika sura ya tano, muhtasari, matokeo ya utafiti, matatizo yaliyojiri katika utafiti na

mapendekezo ya utafiti, yametolewa.

Mwisho wa tasnifu hii ni marejeleo na kiambatisho.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

KAUI, T (2021). Usawiriwa Vijanakatika Tamthilia Teuleza Kisw Ahili. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/usawiriwa-vijanakatika-tamthilia-teuleza-kisw-ahili

MLA 8th

KAUI, TITUS "Usawiriwa Vijanakatika Tamthilia Teuleza Kisw Ahili" Afribary. Afribary, 02 Jun. 2021, https://track.afribary.com/works/usawiriwa-vijanakatika-tamthilia-teuleza-kisw-ahili. Accessed 25 Dec. 2024.

MLA7

KAUI, TITUS . "Usawiriwa Vijanakatika Tamthilia Teuleza Kisw Ahili". Afribary, Afribary, 02 Jun. 2021. Web. 25 Dec. 2024. < https://track.afribary.com/works/usawiriwa-vijanakatika-tamthilia-teuleza-kisw-ahili >.

Chicago

KAUI, TITUS . "Usawiriwa Vijanakatika Tamthilia Teuleza Kisw Ahili" Afribary (2021). Accessed December 25, 2024. https://track.afribary.com/works/usawiriwa-vijanakatika-tamthilia-teuleza-kisw-ahili