IKISIRI
Utafiti huu ulijikita katika kutathmini utayari wa Wakenya katika utekelezaji wa
sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya. Utafiti ulilenga
wakaazi wa mji wa Nairobi hasa katika ofisi za shughuli za kiutawala na vyombo
vya habari vinavyopatikana humo. Utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha ya
Kiswahili umeathiriwa na mambo mbalimbali. Baadhi ya mambo hayo ni kama
vile: hadhi ambayo lugha hii imepewa, manufaa ya lugha hii miongoni mwa
athari nyingine. Malengo ya utafiti huu yalikuwa; kubaini iwapo kuna utayari
katika kutekeleza sera ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi. Na namna utayari
huu utakavyosaidia katika kuimarisha sera hii mpya ya lugha ya Kiswahili hasa
katika urasmi wake, kuchunguza changamoto zinazokabiliwa katika shughuli za
kiutawala na vyombo vya habari kuhusu hadhi mpya ya lugha ya Kiswahili na
mwisho kutambua ni vipi utayari wa utekelezaji katika sera hii unavyoweza
kutekelezwa ili kuweza kufanikisha lengo lake la kuwa lugha rasmi. Utafiti huu
ulitumia mitazamo miwili ya upangaji wa lugha. Tulizingatia upangaji lugha
kihadhi ambao huzingatia juhudi zinazochukuliwa ili kubadilisha matumizi na
majukumu ya lugha katika jamii na mtazamo wa upangaji lugha kifahari
unaolenga kutoa mielekeo chanya ya kisaikolojia ambayo ni muhimu ikiwa
kutakuwepo na ufanisi wa muda mrefu katika upangaji lugha. Utafiti huu
uliongozwa na Nadharia ya Utekelezaji iliyoasisiwa na Spencer (1971). Utafiti
wa kina nyanjani ulifanywa ili kubaini ni changamoto zipi ambazo zinakumba
utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi. Mtafiti
alitumia sampuli finyu ili kupata matokeo bora zaidi. Data ilikusanywa nyanjani
kwa kutumia hojaji na mahojiano ili kubaini mambo yanayohusu utayari wa
utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili hasa baada ya lugha hii kufanywa
lugha rasmi. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia programu ya SPSS.
Kutokana na matokeo ya utafiti ilidhihirika kuwa hakuna usawa katika matumizi
ya lugha yaKiswahili na ile ya Kiingereza. Utafiti ulionyesha kuwa lugha ya
Kiswahili ilitumika sana katika idara ya polisi, Kiingereza kilitumika sana katika
vyombo vya habari. Hata hivyo, ni bora wabunge wapitishe miswada
inayohusiana na lugha ya Kiswahili ili iwe sheria. Utafiti huu utasaidia wadau
wanaohusika na maswala ya sera ya lugha na kuweka mikakati ya kuhakikisha
kuwa inatekelezwa. Mapendekezo yaliyofanywa na mtafiti yakizingatiwa na
kutekelezwa, hadhi ya lugha ya Kiswahili itaweza kuwa bora katika sekta
zilizofanyiwa utafiti kwa nchi nzima kwa ujumla.
NAIROBI, K (2021). Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya. Afribary. Retrieved from https://track.afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya
NAIROBI, KAUNTI "Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya" Afribary. Afribary, 01 Jun. 2021, https://track.afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya. Accessed 05 Nov. 2024.
NAIROBI, KAUNTI . "Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya". Afribary, Afribary, 01 Jun. 2021. Web. 05 Nov. 2024. < https://track.afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya >.
NAIROBI, KAUNTI . "Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya" Afribary (2021). Accessed November 05, 2024. https://track.afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya